ILIBAKI KIDOGO BENZEMA AIHARIBIE REAL MADRID

 Real Madrid imeendelea kutoa vipigo kwa kila mpinzani wake inayekutana naye La Liga. Jumatano hii ilikuwa zamu ya Osasuna wao walikubali kipigo cha mabao 3-1 kwenye mchezo wa raundi ya 33 kwenye ligi hiyo.



Mabao ya Real Madrid yalifungwa na beki mahili David Alaba dakika ya 12 lakini Osasuna walisawazisha kupitia Ante Budimir dakika ya 13 na kuibua ushindani mkali kwa pande zote mbili. Marco Asensio aliipa Real Madrid bao la pili dakika ya 45 na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko Madrid wakiongoza mabao 2-1.

BENZEMA AKOSA PENATI MBILI 

Karim Benzema aligeuka kuwa kituko baada ya kukosa mikwaju miwili ya penati. Dakika ya 52 mchezaji wa Osasuna aliushika mpira ndani ya 18 na refa aliamuru penati lakini kipa Sergio Herrera aliipangua  penati hiyo ya Karim Benzema . Dakika ya 59 mchezaji Rodrygo alichezewa madhambi ndani ya 18 na refa aliamuru penati na jukumu la kuipiga alipewa Karim Benzema lakini kipa wa Osasuna Sergio Herrera alifanikiwa kuicheza .Shukrani za kipekee zimwndee Lucas Vazquez aliyefunga bao la tatu dakika ya 90 ya mchezo huo na kuifanya Real Madrid kubaki kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 78 na sasa wanahitaji pointi 1 tu waweze kutangazwa mabingwa wapya wa La Liga.

Karim Benzema anauwezekano mkubwa wa kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa msimu huu baada ya kufunga mabao 25.Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kutwaa kiatu hicho kilichoshikiliwa na Lionel Messi kwa misimu mitano mfululizo.

Post a Comment

0 Comments