ads

adds

COASTAL UNION YATANGAZA KIAMA KWA SIMBA LEO

 Klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga itawakaribisha mabingwa watetezi wa NBC Premier League  klabu ya  Simba  kwenye mchezo wa ligi kuu raundi ya 19 . Mchezo huu utapigwa dimba la mkwakwani kuanzia saa 10;00 jioni na unategemewa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Simba ataingia uwanjani akiwa na pointi 37 huku mpinzani wake anayeongoza ligi klabu ya Yanga wakiwa na pointi 51 na kuwafanya wawe na tofauti ya pointi 14,kama Simba atashinda mchezo huo basi gepu litapungua kwa pointi 3. Ushindi wa Yanga hapo jana ni kama umeiongezea mzigo mzito klabu ya Simba kuelekea Ubingwa.

Kwa Upande wa Coastal Union wao wanakibarua kigumu zaidi wakijinusuru kushuka Daraja mwishoni mwa msimu huu baada ya kuvuna pointi 21 tu kwenye michezo 18 waliyocheza na kuwafanya washike nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi wenye timu 16.

Kama Coastal watashinda mchezo huo basi watasogea mpaka nafasi ya 8 wakiwa na pointi 24 na kuwafanya wawe na ahueni zaidi. Uwepo wa kocha mkuu Juma Mgunda unaweza kuleta matokeo chanya kutokana na uzoefu wake hasa kwenye mechi ngumu kama hizi.

Mchezo huu ni kama Coastal Union wameanza kuwaharibu wachezaji wa Simba kisaikolojia tangu wawasili Tanga na hilo lilianza kuonekana kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo meza na viti vilivyotumika kwenye mkutano huo vilikuwa chini ya kiwango na kuzua zogo kwa wadau wa soka wakilaumu uongozi wa soka mkoa wa tanga na bodi ya ligi wanaosimamia maandalizi yote ya michezo.

Mashabiki wa Coastal Union wameonekana kujiamini na mmoja wao amenukuliwa akisema "Hapa ndio mkwakwani na leo mnyama atalaruliwa na Mbwa Mwitu,tunahitaji pointi zetu tatu na mchezo huu ni muhimu sana kujiepusha na kushuka daraja ,Simba wajue tu leo wanacheza na Coastal Union halisi na wajiandae kwa kipigo"


Post a Comment

0 Comments