advertise with us

ADVERTISE HERE

CHELSEA YAPIGWA NA BUTWAA DHIDI YA ARSENAL

 Mashabiki wa Chelsea wameendelea kuambulia maumivu makali baada ya kuchezea kipigo cha mabao 4-2 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza.Huu unakuwa mchezo wa 31 kwa Chelsea yenye pointi 62 na mchezo wa 32 Kwa Arsenal wenye pointi 57.Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Stamford Bridge nyumbani kwa Chelsea na Edward Nketiah alikuwa wa kwanza kufunga bao la kwanza dakika ya 13 lakini Chelsea walisawazisha upitia Timo Werner dakika ya 17.

Winga machachali Smith Rowe aliipa Arsenal bao la 2 dakika ya 27 lakini beki mkongwe Azipilicueta alisawazisha bao hilo dakika ya 32 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mason Mount.Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko matokeo yalikuwa ni 2-2.

Kipindi cha pili kilianza na Arsenal walionyesha umakini mkubwa eneo la ulinzi na kuongeza mashambulizi yaliyozaa bao la 3 lililofungwa na Edward Nketiah dakika ya 57 ya mchezo huo huku Bukayo Saka akifunga bao la nne kwa mkwaju wa penati dakika ya 92.

matokeo hayo yanaifanya Arsenal kupanda mpaka nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi na Chelsea kuendelea kusalia nafasi ya 3 kwenye ligi hiyo.

Post a Comment

0 Comments