BADO MECHI NNE TU MADRID AWE BINGWA

 Real Madrid wanajiandaa kutwaa taji la La Liga kwa mara ya 35 tangu walipoanza kushuriki michuano hiyo mwaka 1929. Kwa msimu wa 2021/22 klabu hii imekuwa moto wa kuotea mbali baada ya kuvuna pointi 72 kwenye michezo 31 waliyocheza.

Ushindi wa mabao 2-0 unaisogeza Madrid katika nafasi ya kutwaa ubingwa na Mpaka sasa klabu hiyo imetawala kila sekta kuanzia mfungaji bora ambaye ni Karim Benzema mwenye mabao 24 na assist 10,timu yenye wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa ambayo ni 37,ushindi wa mechi nyingi za ugenini na nyumbani.

Madrid wanahitaji mechi 4 tu waweze kutangazwa mabingwa wapya wa La Liga ,nafasi ya 2 inashikiliwa na Sevila mwenye pointi 60 baada ya michezo 31 na bingwa mtetezi Atletico Madrid akiwa nafasi ya 4 akiwa na pointi 57 baada ya mechi 57.

Post a Comment

0 Comments