Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imefanya maamuzi sahihi ya kumuongezea mkataba kocha wake Pitso Mosimane. Kocha huyo mwenye miaka 57 ataendelea kuwepo klabuni hapo mpaka mwaka 2024.
Pitso Mosimane mzaliwa wa Afrika Kusini alijiunga na Al Ahly akitokea Mamelodi Sundowns mwaka 2020 baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa 2019/20. na tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Misri ameweka rekodi mbalimbali ikiwemo kutwaa kombe la CAF CHAMPIONS LEAGUE mara mbili mfululizo,kuvaa medali za shaba kwenye michuano ya klabu bingwa dunia,The Egypt Cup mara 1 na CAF Super Cup mara 2
Historia fupi ya kocha Mosimane
Kocha Mosimane alianza maisha ya ukocha mwaka 2001 akiitumikia Super Sport United mpaka mwaka 2007 na alijiunga na timu ya taifa ya Afrika Kusini kama kocha msaidizi mpaka mwaka 2010 kisha kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa hilo mpaka mwaka 2012. Mwaka 2012 alijiunga na Mamelodi Sundowns mpaka mwaka 2020 kama kocha mkuu kisha kutimkia Al Ahly .
Mosimane anatajwa kama kocha mwenye mafanikio zaidi kwa Afrika kutokana na rekodi zake kwenye michuano mbalimbali anayoshiriki.mkataba mpya wa kusalia Al Ahly mpaka mwaka 2024 unazidi kumfanya awe kocha mwenye dhamani zaidi kwa Afrika.
0 Comments