BENZEMA AIPELEKA REAL MADRID ROBO FAINALI KISHUJAA

 Karim Benzema ameendelea kuwa mwiba mkali kwa wapinzani wa Real Madrid kwa msimu wa 2021/22. Nyota huyu wa Ufaransa mwenye miaka 34 ameudhihirishia ulimwengu kwamba yeye ni bora nyakati zote baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya Paris Saint Germain kwenye mchezo wa 16 bora.


Benzema alifunga bao la kuongoza dakika ya 61 huku akifunga la pili dakika ya 76 na bao la tatu dakika ya 78 na kumfanya ashike nafasi ya tatu akifungamana na Mohammed Salah kwa kuwa na mabao 8 huku Robert Lewandowski akiongoza kwa mabao 12 nafasi ya pili inashikiliwa na Haller kutoka Ajax akiwa na mabao 11.

Hat Trick dhidi ya PSG inakuwa ya tatu kwa Benzema tangu aanze kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.Ronaldo na Messi ni wachezaji pekee wenye Hat trick 8 huku Robert Lewandowski akiwa na Hat Trick 5 kwenye michuano hiyo.

Kwa upande wa ligi kuu Hispania Benzema ameisaidia timu yake kuongoza msimamo kwa kufunga mabao 20 na kutengeneza mengine 10 kwenye mechi 27 walizocheza na kumfanya awe mchezaji anayeongoza kwa mabao ya kufunga na kutengeneza mpaka sasa.

Post a Comment

0 Comments