AUBEMAYANG AMETUA BARCELONA NYAKATI SAHIHI

 Barcelona wamelamba dume kwa msimu huu baada ya kumnasa mshambuliaji Piere Aubemayang.Nyota huyu amekuwa akionyesha kiwango cha hali ya juu tangu alipojiunga Barcelona akitokea Arsenal kwa mkopo. Mpaka sasa PIere amekwishafunga mabao 7 kwenye michezo saba aliyocheza ndani ya Barcelona na tayari ana hat trick 1.

Kwa msimu wa 2021/22 Nyota huyo akiwa arsenal alishindwa kabisa kuendana na mfumo wa kocha wake Mikel Arteta na kumpelekea kukaa benchi kwa baadhi ya mechi. Wengi walisema kiwango cha Aubemayang kimefika kikomo na hastahili kuendelea kubaki Arsenal. 

Safari kuelekea Barcelona 

Kuondoka kwa mshambuliaji tegemezi Lionel Messi mwishoni mwa msimu wa 2020-21 kulipelekea Barcelona kuanza vibaya msimu wa 2021/22 wakiondolewa katika michuano ya copa del ley, wakitolewa hatua ya makundi uefa na kupelekwa europa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 20 huku wakiachwa mbali kabisa kwenye kinyang'anyilo cha kombe la ligi la liga na mahasimu wao Real Madrid . 

Tangu Barcelona wamsajili nyota huyo kipindi cha dirisha dogo mambo yamebadilika kwa upande wao na sasa timu imerejea kwenye ushindani. Kwa upande wa Pierre amekuwa moto mkali na wachambuzi wameanza kumtabiria neema ya kuwa na mafanikio ndani ya Barcelona kwa eneo la ushambuliaji kama Luis Suarez, david villa, Thiery Henry na Sanchez Alexis waliowahi itumikia klabu hiyo. 

Amospoti kwa kushirikiana na Amostudios tunakuandalia makala safi kabisa itakayoonekana ndani ya amospotixtra mwanzoni mwa april tukiwachunguza nyota mbalimbali wa kiafrica wanaofanya maajabu ulaya 

Post a Comment

0 Comments