Klabu ya Mbeya City imekwishawasili jijini Dar es salaam kukabiliana na Mabingwa wa kihistoria klabu ya Dar Young Africans (YANGA SC) mchezo wa ligi kuu NBC utakaopigwa dimba la mkapa hapo kesho majira ya saa 1;00 usiku
Mchezo huu unategemewa kuwa wa aina yake kutokana na timu hizo kuwa na wasaa mzuri wa kujiandaa lakini kubwa zaidi ni klabu ya Yanga kuwa na rekodi ya kipekee kwa msimu huu baada ya kucheza michezo 13 bila kufungwa na wakivuna pointi 35
Mbeya City wao wapo nafasi ya 4 wakiwa na pointi 22 wakicheza michezo 13. Kikosi hicho kimeonekana kuwa gumzo msimu huu baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi walizocheza huku kujiamini kwa wachezaji kukiongezeka baada ya kuifunga Simba bao 1-0 na kuwafanya wawe tishio uwanjani .
Mbeya City kwa mechi 5 zilizopita imeibuka tishio baada ya kufungwa mchezo mmoja tu dhidi ya Coastal union huku wakiibuka na ushindi dhidi ya Simba na Dodoma Jiji Sare dhidi ya Azam fc na Polisi Tanzania.
Mashabiki wa Simba wanatamani Mbeya City amfunge Yanga ili kupunguza utofauti wa pointi kwenye msimamo wa ligi.Simba wanapointi 28 huku Yanga wakiwa na pointi 35 sawa na utofauti wa alama 7. Mbeya City inatakiwa inatakiwa kupambana na kushinda mechi zake ili kurejea nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.Kama Mbeya City watashinda mchezo huo basi watakuwa na pointi 25 wakishika nafasi ya 3 na kama Yanga watashinda basi watakuwa nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 38 wakiwazidi Simba pointi 10.
MATOKEO YA MECHI TANO ZA MBEYA CITY
0 Comments