Moja kati ya wachezaji wa kigeni waliobahatika kuzitumikia klabu za Simba na Yanga kwa mafanikio makubwa ni Benard Morrison. Mchezaji huyu alijiunga na Klabu ya Simba akitokea Yanga alikodumu kwa miezi 6 tu.
Historia fupi ya Morrison
Mchezaji huyu raia wa Ghana alianza maisha ya soka la kulipwa kwa kuitumikia Heart of Lions mwaka 2011-13 kisha alijiunga na Ashanti Gold mwaka 2013 hadi mwaka 2015 na baadaye kutua As Vita 2015-16.
Morrison alijiunga na Orlando Pirates msimu wa 2016-18 na baadaye alitua nchini Congo kuitumikia DC Motema pembe kwa msimu wa 2018-19.
Alifikaje Tanzania
Msimu wa 2019-20 alijiunga na klabu ya Yanga kwa mkataba wa miezi 6 na ndani ya kipindi hicho alionyesha uwezo mkubwa mno na mwisho wa msimu aliachana na klabu hiyo kwa mgogoro na mgogoro huo ulipelekwa CAS (Mahakama ya michezo) na mwaka 2021 Ulitolewa Uamuzi kwamba mchezaji huyo .alikuwa huru baada ya kumalizana na Yanga.
Msimu wa 2020-21 Morisson alijiunga na Simba SC kama mchezaji huru na alicheza kwa mafanikio makubwa mno huku akiisaidia timu hiyo kutwaa mataji ya ligi kuu,FA ,Kombe la Mapinduzi na kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa Africa.
Kinachommaliza Morrison
Mbali na kuwa na kipaji cha kipekee lakini mchezaji huyu hana Nidhamu kabisa hususani nje ya uwanja.Mara kadhaa inaripotiwa Morrison amekuwa akitoroka kambini na hata kuleta utukutu kwa viongozi wake hasa mikataba yake inapokaribia kuisha.
Kitendo cha kucheza kwenye klabu 7 tofauti ndani ya miaka 11 ni ishara kwamba mchezaji huyo hajitambui na hajui ni nini haswa anachokitaka kwenye kazi yake. Mara kadhaa amekuwa akipata kashfa kuanzia Nchini Afrika kusini aliposhutumiwa kwa kesi ya kununua gari la wizi.
Kushutumiwa na klabu ya Yanga kwamba alishasaini mkataba mpya na Simba ilihali anaitumikia Yanga. kutoroka kambini na kuonekana maeneo ya Starehe na wanawake mastaa wa tanzania ni dhahiri amekuwa mtovu wa nidhamu.
Hitimisho
Mpaka May 2022 Morrison atakuwa anafikisha miaka 29 ,Je kuna mtu amemkumbusha hilo Morrison,kwa mchezaji wa kawaida hasa Africa hustaafu ndani ya miaka 32-34.kama Morrison ataendelea na masikhara yake basi atakuwa ni mmoja ya wachezaji waliowahi kuwa na vipaji vikubwa ila hawakunufaika navyo.Na kwa mwendo anaokwenda nao hawezi kufika popote kisoka.
0 Comments