MORRISON ANAIHITAJI SANA SIMBA KULIKO SIMBA INAVYOMUHITAJI

 Kuna wakati sifa za nje ya uwanja zikizidi basi huharibu kila kitu ndani ya uwanja.Benard Morrison anaamini bila yeye Simba haiwezi kufanya lolote.Anaamini bila yeye Simba itakuwa na maisha magumu jambo ambalo si kweli.Kwa msimu wa 2021-2022 Simba imekuwa ikiwategemea zaidi Kibu Dennis,Dilunga ,Benard Morrison,Sakho,Mhilu na Jimson kama mawinga.Utitiri huu wa mawinga unamfanya kocha pablo abadili wachezaji hao mara kwa mara kwa mfumo wa Rotation na mara zote amekuwa akipata matokeo.

Mechi nyingi Morrison amekuwa akitokea benchi na hiyo ni ishara kwamba ni mchezaji wa akiba na atahitajika  pale mchezaji aliyeanza amechoka au timu inapokuwa inatafuta ushindi kilazima. Kwa akili ya kawaida ni kuwa mchezaji kama huyo hana nafasi kikosi cha kwanza na hata anapokosekana timu haiwezi kuyumba.

Kurejea kwa Clatous Chama kunawafanya Simba waamini mchezaji huyo ni muhimu zaidi kuliko mchezaji yeyote na hilo amelionyesha kwenye mechi tatu alizocheza tangu kurejea.Morrison asijidanganye kuwa yeye ni zaidi ya Simba au yeye ni mfalme ndani ya timu hiyo na kudhani kuondoka kwake kutaleta mtikisiko ndani ya Simba .

Kitendo cha kusimamishwa kwake na timu haijaonyesha tofauti yoyote kiuchezaji ni ishara kwamba nafasi yake imekwishazibwa na hata atakapoondoka basi tusitegemee kuona utofauti wowote kiuchezaji kwa upande wa Simba,

Kwa sasa Simba inakwenda kucheza michuano ya kombe la Shirikisho Afrika na huu ni wakati ambao Morrison alipaswa kutuliza akili akaonyesha uwezo wake wote na kupata mkataba mnono ndani ya Simba au klabu zingine kumnunua kwa pesa ndefu ila kitendo cha kusimamishwa na klabu hiyo kutamnyima nafasi nyota huyo na hata kama ataondoka mwisho wa msimu basi atajiona alichezea shilingi kwenye shimo la choo ilihali Simba walimwamini mno.


Post a Comment

0 Comments