BETI NASI UTAJIRIKE

AZAM WAENDELEZA KIPIGO WATUMA SALAM SIMBA

 Klabu ya Azam FC yenye makazi yake Chamazi jijini Dar es salaam wameendelea kuonyesha ubabe baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji.



Azam walijipatia bao la kuongoza kupitia mshambuliaji wake hatari Rodgers Kola dakika ya 5 ya mchezo huku dakika ya 64 Idris Mbombo akitupia bao la 2 .Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Moallin kimeonyesha uwezo mkubwa tangu kocha huyo alipokabidhiwa rasmi kukinoa. Ni siku chache zimepita tangu timu hiyo kuibuka na ushindi mnono wakiwa ugenini k wa mabao 4-0 dhidi ya Prisons 

Kwa sasa Azam inashika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 24 baada ya michezo 14 nyuma ya Simba wenye pointi 28 baada ya michezo 13. Azam wamebadilika na wamezidisha makali na hii inawafanya waanze kuwa tishio kuelekea mbio za ubingwa.

Yanga wanapointi 35 na wanapaswa kukaza zaidi kwani vilabu kama Azam na Simba vimerejea kwenye form na kama watalegea basi mbio za za ubingwa zitakuwa ngumu.

Post a Comment

0 Comments