advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA WATOA SABABU ZA KUHAMISHA MECHI NA MBAO FC

 Mashabiki wa Yanga mkoani Mwanza wajiandae kupata burudani ya aina yake baada ya timu hiyo kuhamishia mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mbao FC jijini humo.


 Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa dimba la Mkapa Dar es salaam lakini uongozi wa Yanga uliomba mchezo huo kuhamishiwa Mwanza ili waweze kupeleka burudani mkoani humo. Naye Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema

"Uongozi uliliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuomba mabadiliko ya uwanja tayari majibu ya ombi hilo yamerudishwa sasa ni rasmi Yanga na Mbao itachezwa Kirumba," alisema.

Wakati huohuo Hafidh alisema baada ya mapumziko ya siku moja mastaa wa timu hiyo wanatarajia kurudi kambini leo tayari kwa maandalizi ya mchezo huo ambao amesisitiza kuwa ni muhimu kwao kupata matokeo ili waweze kusonga hatua inayofuata.

"Hakuna muda wa kupoteza tuna siku chache za maandalizi kabla atujasafiri kwenda Mwanza kusaka pointi tatu muhimu ambazo zitatuwekea mazingira mazuri kupambania nafasi ya kutwaa taji la kombe la Shirikisho," alisema Hafidh.

Post a Comment

0 Comments