advertise with us

ADVERTISE HERE

WATATU WAPIGWA CHINI SIMBA SAFARI YA ZANZIBAR

 Hatimaye kikosi cha Simba kimeondoka jijini Dar es salaam kuwasili zanzibar kwenye michuano ya kombe la mapinduzi kwa mwaka 2022. Msafara huo umeondoka leo saa 3 asubuhi na kufika saa 6 mchana.


 kukiwa na wachezaji wa kikosi cha kwanza na chapili lakini kumekosekana wachezaji watatu akiwemo Bernard Morrison aliye kwao Ghana kwa masuala ya kifamilia ,Aishi Manula na Joash Onyango ambao wote wameachwa jijini Dar es salaam.

Tadeo Lwanga ni mmoja wa nyota waliosafiri na timu hiyo baada ya kurejea akitokea majeruhi Taddeo  aliyekuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutokana na majeraha ya mguu yalikuwa yakimsumbua mpaka kurudi kwao kwa matibabu zaidi.

Kocha wa Simba, Pablo Franco amesema kikosi cha Simba kinakwenda katika mashindano hayo kikiwa na mlengo wa kuchukua taji hilo la kwanza msimu huu kwani ni miongoni mwa mafanikio wanayotamani kuyapata chini yake.

Pablo amesema Lwanga ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika msafara huo kutokana maendeleo yake ni mazuri na anategemea kumtumia katika mashindano hayo ili kuona namna gani atarudi katika hali ya ushindani.

"Maandalizi yetu katika mashindano haya ni mazuri ndio maana tunakwenda na kikosi kizima ili kupata uwanja mpana wa kutumia wachezaji wote kwa nyakati tofauti kulingana na mechi zitakavyokuwa," amesema Pablo.Post a Comment

0 Comments