BETI NASI UTAJIRIKE

UCHAMBUZI; USIYOYAFAHAMU KUHUSU KUNDI B AFCON

 Michuano ya 33 ya Kombe la Mataifa ya Afrika inaanza nchini Cameroon, Jumapili Januari 9, ikiwa imecheleweshwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la corona.



Hapa, tunaangazia kundi B, ambalo linajumuisha waliokuwa namba mbili mwaka 2019 Senegal, Zimbabwe, Guinea na Malawi

Ratiba

JumatatuJanuari 10; Senegal v Zimbabwe, Guinea v Malawi

IjumaaJanuari 14: Senegal v Guinea, Malawi v Zimbabwe

Senegal

Sadio Mane in action for Senegal

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

 Kubakia nafasi ya juu Afrika katika orodha ya dunia ya Fifa kwa miezi 36 ni rekodi na uthibitisho wa uthabiti.

Bado, matokeo yoyote kando na kuwa mabingwa yatachukuliwa kuwa kushindwa kwa Senegal, waliofika fainali mwaka 2019. Shirikisho hilo lilimkumbusha wazi kocha mkuu Aliou Cisse kuhusu lengo hilo huku kandarasi yake ikiongezwa hadi Kombe la Dunia la mwaka 2022.

Tangu michuano hiyo ifanyike nchini Misri, uti wa mgongo wa timu hiyo haujabadilika sana huku Edouard Mendy akiwa mlinda mlango, nahodha Kalidou Koulibaly akiwa kiongozi wa safu ya ulinzi, Idrissa Gana Gueye katika safu ya kati na Sadio Mane akiwa tishio kuu la mashambulizi.

Hata hivyo kikosi kinaweza kukumbwa na tatizo kwani msimu wa winga wa Monaco, Krepin Diatta tayari umekwisha baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti huku nyota mwingine anayeibuka, Ismaila Sarr wa Watford, naye akiuguza jeraha la goti na huenda akakosa kuanza kwa michuano hiyo.

Miaka 20 baada ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza, Senegal wanatumai hatimaye kuleta kombe nyumbani.

Zimbabwe

Knowledge Musona in action for Zimbabwe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambulizi wa Al Tai na Zimbabwe Knowledge Musona ni nahodha wa kikosi kilichokumbwa na majeraha na machafuko ya FA

Steve Vickers (Mwandishi wa Habari za Michezo, Harare): Zimbabwe inaingia katika Kombe lao la tano la Mataifa ya Afrika ikiwa na changamoto kwenye bodi ambazo zinahatarisha kupigwa marufuku kushiriki soka la kimataifa. Bodi ya ya shirikisho la soka nchini himo (Zifa) ilisimamishwa hivi karibuni na hata kudai uteuzi wa Norman Mapeza kuwa kocha si halali.

The Warriors wamekumbwa na majeraha ya wachezaji muhimu akiwemo kiungo Marvellous Nakamba (Aston Villa), Brendan Galloway (Plymouth) na Marshall Munetsi (Reims), huku Khama Billiat mwenye ushawishi mkubwa akitangaza kustaafu kutokasoka ya kimataifa mwezi Novemba.

Hii inawaacha nahodha Knowledge Musona, anayecheza Saudi Arabia, na mshambuliaji wa Lyon Tino Kadewere kama majina makubwa zaidi kikosini.

Zimbabwe wana ushindi mmoja pekee kati ya mechi 18 zilizopita katika michuano yote - ushindi wa ugenini nchini Botswana ambao ulichangia wao kufuzu.

Ushindi wao wa mwisho katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ulikuwa wa 2-1 dhidi ya Ghana mnamo 2006, huku kampeni za 2017 na 2019 zikiwafanya kupata pointi moja mara zote mbili. Inaonekana kama fainali nyingine ngumu.

Guinea

Naby Keita in action for Guinea

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Naby Keita anatarajiwa kuchuana na mwenzake wa Liverpool Sadio Mane wakati Guinea itakapomenyana na Senegal Januari 14.

Cellou Tata (mwandishi wa habari za michezo huko Conakry): Hali ya wasiwasi imejaa Guinea, baada ya kufuzu kwa Kombe la Dunia kulikokumbwa na changamoto. Kocha Didier Six alifukuzwa kazi baada ya michezo mitatu na naibu wake, mchezaji wa zamani wa kimataifa Kaba Diawara, akachukua wadhifa huo.

Bado kushinda mechi hata moja, kazi inayowangoja ni kubwa. Hatuko mbali na mazingira ya Kombe la Mataifa lililopita, ambapo timu hiyo ilitolewa katika awamu ya 16 bora na walioibuka mabingwa Algeria.

Changamoto kwa Kaba Diawara itakuwa kuwa na ujasiri wa kuwaweka kando baadhi ya "watendaji" kwa ajili ya timu - kama alivyoonyesha kwa kumuondoa Camara kwenye kikosi chake.

Baada ya Fifa kuteua kamati ya Shirikisho la Soka la Guinea, lengo la kwanza litakuwa kufikiria jinsi ya kuepuka sarakasi za 2019.

Malawi

Charles Petro in action for Malawi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa Malawi Charles Petro anachezea Sheriff Tiraspol ya Moldova

Frank Kandu (Mwandishi wa Soka nchini Malawi): Malawi watakuwa wanashiriki kwa mara ya tatu kwenye kinyanganyiro kikubwa zaidi cha soka barani. Katika mechi za awali mwaka 1984 na 2010, walishindwa kupita awamu ya makundi.

Meck Mwase aliongezewa mkataba wa miaka miwili na kuwa kocha wa tatu kuiongoza nchi hiyo katika fainali hizo, lakini tangu kufuzu timu hiyo imekumbwa na changamoto.

Flames ilishinda mechi moja tu kati ya sita za makundi katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022 - matokeo ambayo yalilazimu mabadiliko ya haraka na Chama cha Soka cha Malawi. Mario Marinica aliteuliwa kuwa mkuu wa jopo la ufundi la Malawi huku Mwase akishushwa cheo na kuwa kocha msaidizi.

Marinica anaamini Malawi inaweza kuwashinda timu kama Zimbabwe na Guinea lakini ana kazi kubwa ya kuifanya timu yake kuwa tayari kwa hatua hiyo kubwa.

Post a Comment

0 Comments