TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE TAREHE 04.01.2022

 Real Madrid, Paris St-Germain, Bayern Munich na Juventus wote wameanzisha mazungumzo na wawakilishi wa Antonio Rudiger kuhusu makubaliano ya awali ya mkataba na beki huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28, ambaye mkataba wake na Chelsea unakamilika msimu wa joto. (Sky Sports)Lille wameambia Newcastle kwamba Mholanzi Sven Botman, 21, hauzwi baada ya klabu hizo kujadili bei ya karibu pauni milioni. (Telegraph - subscription required)

Lakini Newcastle wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Atletico Madrid juu ya kumsajili beki wa Uingereza Kieran Trippier, 31, wanapokaribia kukubaliana bei ya pauni milioni 25. (Express)

Kieran Trippier

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa Atletico Madrid NA Uingereza Kieran Trippier

Mzungumzo ya Chelsea ya kurefusha mkataba wa Andreas Christensen, 25, yamegonga mwamba kwa mara nyingine, huku Barcelona wakionesha ishara ya kutaka kumnunua mlinzi huyo wa Denmark mwezi huu wa Januari ijapokuwa mkataba wake na Chelsea unakamilika msimu wa joto. (Gianluca Di Marzio - in Italian)West Ham wamefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Brazil Gabriel Barbosa, 25, kutoka Flamengo. (Sky Sports)

Roma wamewasilisha dau la kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, kwa mkopo kutoka Arsenal hadi mwisho wa msimu na chaguo la kumnunua msimu wa joto. (Athletic - subscription required)

Beki wa Scotland Nathan Patterson, 20, anajiandaa kufanya vipimo vya matibabu na Everton baaada ya Rangers kukubali dau la awali la pauni milioni 12 , ambalo huenda likaongezeka hadi pauni milioni 16 ikijumuishwa na marupurupu mengine. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 34, anataka kuondoka Atletico Madrid wakati mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto kwa matumaini ya kujiunga tena na mshambululiaji mwenza wa Argentina Lionel Messi, 34 anayechezea Paris St-Germain. (El Nacional - in Catalan)

Luis Suarez

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Luis Suarez has scored twice since joining Atletico Madrid

Rais wa Barcelona Joan Laporta amesema klabu hiyo "wamerudi kama wachezaji wakubwa" alipozungumza kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, kutoka Borussia Dortmund.(Mirror)

AC Milan wanafanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Ureno Renato Sanches, 24, kutoka Lille. (Calciomercato - in Italian)

Post a Comment

0 Comments