ads

adds

STAA WA YANGA KUREJEA DIMBANI HIVI KARIBUNI

Mashabiki wa Yanga wamefurahishwa baada ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Yacouba Songne raia wa Burkina Faso kuanza mazoezi mepesi, huku akitarajiwa kurejea rasmi uwanjani baada ya mwezi mmoja kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote.


Yacouba alipata majeraha ya goti 
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Novemba 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na Yanga kushinda 3-1.

Baada ya kuumia, Novemba 10, mwaka huu Yacouba alipelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu akiongozana na Dokta wa Viungo wa Yanga, Youssef Mohamed, huku taarifa za awali kutoka kwa daktari zikieleza atakaa nje kwa muda wa zaidi ya miezi minne.

Dokta Youssef alinukuliwa akisema: “Kila kitu kipo sawa, kuhusu hali ya Yacouba kwa sasa anaendelea vizuri.


Post a Comment

0 Comments