YANGA YASAMBARATIKA SIMBA WASHINDWE WAO TU ZANZIBAR

 Wakati Simba ikishusha nyota wote wa kikosi cha kwanza kwenye michuano ya Mapinduzi Cup hali ni tofauti kwa mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Yanga baada ya kupeleka kikosi cha kitofautiYanga inaondoka leo jioni kuelekea Zanzibar lakini itawakosa nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo Nabi aliyetimkia Ubelgiji. Kabla ya kuondoka hapo jana asubuhi kocha huyo amenukuliwa akisema.

Nimewapa ruhusa (Mayele na Aucho) wameomba kwenda makwao kukutana na familia zao,. nimewaambia ndani ya siku saba wawe wamerejea nchini kuendelea na programu niliyoiacha,” alisema

 Nabi ameiongoza Yanga msimu huu kushinda mechi tisa za Ligi Kuu Bara na kutoka sare mbili ikikusanya pinti 29 katika mechi zao 11 ilizocheza hadi sasa.

Mayele na Aucho waliondoka nchini juzi kila mmoja akirejea nchini kwake kwa mapumziko na kufanya sasa Yanga kuwakosa mastaa wake watano wa kikosi cha kwanza, akiwamo kipa Diarra Djigui aliyepo kikosi cha Mali kitakachoshiriki Fainali za Afrika (Afcon), beki Djuma Shaban, Mukoko Tonombe na Yannick Bangala walioenda kujiunga na kikosi cha DR Congo kitakachoshiriki pia fainali za Afcon huko Cameroon kuanzia Januari 9.

Post a Comment

0 Comments