BETI NASI UTAJIRIKE

PABLO FRANKO MARTIN AKALIA KUTI KAVU SIMBA

 Kocha mkuu wa klabu ya Simba Parblo Martin ameendelea kuwa na wakati mgumu baada ya timu hiyo kuendelea kufanya vibaya ligi kuu NBC. Kocha huyo amejikuta kuwa na wakati mgumu baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.


Kocha huyo ameiongoza Simba kwenye michezo 13 ya ligi kuu na ameshinda michezo 8 akitoka sare 2 na kufungwa 2 akikusanya  pointi 25.Simba haijapata ushindi tangu iliporejea kutoka Zanzibar kwenye kombe la Mapinduzi ambako waliibuka mabingwa wa michuano hiyo

Mambo yalianza kuharibika kwenye mchezo wa 11 dhidi ya Mbeya City wakiwa dimba la Sokoine Mbeya Simba walifungwa bao 1-0  na baada ya hapo walielekea Morogoro kuvaana na Mtibwa Sugar mchezo wa raundi ya 12 uliomalizika kwa sare ya 0-0  katika dimba la Manungu. 

Simba walielekea Bukoba kuvaana na Kagera Sugar mchezo wa raundi ya 13 na wameambulia kipigo cha bao 1-0.

Matokeo haya matatu yanaifanya Simba kukusanya pointi 1 na kusalia nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi nyuma ya watani zao wa jadi Yanga. Mpaka sasa uongozi wa Simba haujasema jambo lolote ila wachunguzi wa mambo wanasema mwisho wa pablo kuondoka Simba umewadia 

Post a Comment

0 Comments