Hatimaye klabu ya Azam FC yenye makazi yake Chamazi Dar es salaam imejiridhisha na kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha Abdi Hamid Moalin. Kocha huyo aliyechukua nafasi ya George Lwandamina.
Moalin alijiunga na klabu hiyo kama mkurugenzi wa ufundi na maendeleo ya vijana na baadaye alipewa nafasi ya kukaimu ukocha mkuu akishikilia mikoba ya Lwandamina ambaye aliondoshwa kutokana na mwenendo mbovu wa Azam FC hasa kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania Bara.
Mara baada ya kukaimu nafasi hiyo Moalin alicheza michezo 2 ya ligi kuu na baadaye kuelekea kwenye michuano ya mapinduzi Cup Zanzibar ambako huko walifanikiwa kushika nafasi ya pili baada ya kufungwa bao 1-0 na Simba SC fainali. Klabu hiyo ilirejea Dar es salaam kuendelea na mechi za ligi ambapo hivi karibuni kikosi hicho kilishinda mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons
Uongozi wa Azam FC chini ya mkurugenzi Popat umeridhishwa na uwezo kocha huyo Mmarekani mwenye asili ya Somalia na wamempa mkataba wa miaka 3.
0 Comments