MRITHI WA MANARA APATIKANA SIMBA,MASHABIKI WAPIGWA BUTWAA

 Hatimae klabu ya Simba imefanikiwa kumtangaza rasmi mrithi wa Haji Manara. ni Ahmed Ally aliyekuwa akiitumikia Azam Media kama mtangazaji. 


Ujio wa Ahmed Ally unakwenda kuongeza nguvu katika idara ya habari ndani ya kikosi cha Simba kutokana na umahiri wake aliouonyesha kama mtangazaji wa vipindi ndani ya Azam sports hasa katika kipindi chake cha mshike mshike viwanjani.

Baadhi ya wadau wamesema Ahmed Ally ni mtu sahihi kwa sasa kushikilia nafasi hiyo kwani ni mtaalamu katika soka lakini pia ni mwandishi wa habari aliyekwishatengeneza jina lake hasa kwa kazi nzuri alizozifanya pale Azam TV.

Awali Baraka Mpenja na Antonio Nugaz walihusishwa kuwa wasemaji wa klabu hiyo lakini  kutangazwa kwa Ahmed Ally ni kidhibitisho cha kuwa Simba haiendeshwi kisiasa bali kitaaluma zaidi.

Mashabiki wa Simba wameonekana kushtukizwa na habari hiyo kutokana na usiri mkubwa uliofanywa na viongozi wa klabu hiyo  kuanzia kumtafuta na kumtangaza msemaji huyo huku wakimsifu CEO wao Barbara Gonzalez kwa uendeshaji wa taasisi hiyo kwa umakini kubwa

Post a Comment

0 Comments