BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAPATA MUAROBAINI WA MASHABIKI WA MCHONGO

 Klabu ya Yanga leo hii tarehe 05.01.2022 imeingia mkataba na makampuni mawili kwa ajili ya kutengeneza mfumo utakaowatambua mashabiki na kurahisisha ulipiaji wa ada mbalimbali na viingilio



Yanga wameingia mkataba na KILINET ambao watasimama kama Mshirika wa Teknolojia (technological partner) na N-CARD wao watakuwa na kazi za kutengeneza kadi mpya za mashabiki wa Yanga.

KILINET

Kampuni hii ya Teknolojia imekubaliana na klabu ya Yanga kutengeneza mfumo tambuzi wa mashabiki na utunzaji taarifa .Mashabiki wa yanga watatakiwa kujisajili kwenye mfumo huu mpya na taarifa zao zitaunganishwa na N-Card zikiwa na majina na picha za kila mwanachama. 

Mfumo huu umegawanyika katika awamu tatu ya kwanza ni hii ya utambuzi wa mashabiki na usajili,hatua ya pili KILINET watatoa application ya Simu ambayo  itakuwa na maudhui ya klabu ya Yanga na hatua ya tatu ni Yanga uchakataji wa maudhui ya klabu ya Yanga .

N-CARD 

Ni shirika la kiserikali lenye wajibu wa kuuza tiketi za viingilio kwenye mechi za ligi kuu na timu ya taifa. N-CARD watapokea taarifa za mashabiki kutoka mfumo wa  KILINET na watachapisha kadi ya mwanachama yenye picha na majina yake halisi.

Jukumu la pili ni uchapishaji kadi za aina mbili za Yanga ambazo moja itakuwa ni kadi ya wanachama wa Yanga itakuwa na rangi ya njano na kadi ya pili ni ile ya mashabiki wa Yanga itakayokuwa na rangi ya kijani. Kadi hizi zitatumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kununua tiketi za mechi za Yanga ,kufanya malipo ya Serikali hasa vivukoni kama kivuko cha Kigamboni na Magogoni.Kadi hiyo itamsaidia Mwanachama kuingia kwenye mikutano mbalimbali ya klabu hiyo.

Huu ni mwendelezo wa mabadiliko ndani ya Yanga kujiendesha kidijitali huku ikitambua mashabiki na wanachama lakini pia kujiongezea kipato chake. Mfumo huu mpya wa Yanga utawafanya wale wanaojiita mashabiki na wanachama wa Yanga kutambulika rasmi huku mamluki wote wakiumbuliwa na kuondolewa  ndani ya Yanga.  Zoezi la utiaji saini ndani ya klabu hiyo limefanywa na Makamu mwenyekiti wa Yanga Bw.Fredrick mwakalebela na Wawakilishi kutoka N Card na KILINET


Post a Comment

1 Comments

  1. Gambling in Vegas | DrmCDC
    Vegas gambling is 김해 출장안마 illegal in the 용인 출장안마 United States, but you can gamble 동해 출장마사지 in Vegas, too. You'll need a sportsbook 울산광역 출장안마 that accepts bets at licensed gambling 천안 출장샵 sites.

    ReplyDelete