MASHABIKI NJIA PANDA KUHUSU HATMA YA KOCHA NABI

Mashabiki wa klabu ya Yanga wameanza kupata wasiwasi baada ya taarifa zisizo rasmi za kuhusu kusepa kwa kocha mkuu wa timu hiyo  Nasreddine Nabi Kocha huyo alipata wakati mgumu wakati anaanza kibarua chake Jangwani kabla ya kupenyeza falsafa zake zinazoifanya sasa Yanga kucheza soka tamu la pasi nyingi na kushambulia sana, huku ikigawa dozi kwa wapinzani ndani ya ligi.

Hata hivyo, taarifa ni kwamba kocha huyo anatarajiwa kumaliza mkataba wake Juni 30 mwaka huu na hadi sasa huku ikielezwa tayari mezani mwake ana ofa tatu kutoka nje ikiwamo klabu yake ya zamani ya El Merrikh ya Sudan.

Mbali na kocha huyo mkataba wake kuelekea ukingoni, lakini hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanza baona ya Nabi na mabosi wa klabu hiyo.

 Nabi amepokea ofa zaidi ya timu tatu kutoka nje ya nchi ikiwamo El Merrikh aliyokuwa akiinoa kabla ya kupigwa chini mapema mwaka jana akiwa ameitumikia kwa muda wa siku 38 tu na kutua Jangwani.

 Nabi alisema kwa kocha yeyote anayefanya vizuri katika timu anayofundisha, lazima kutakuwa na nyingine zinazomhitaji na anategemea hilo hata kwa upande wake.

Post a Comment

0 Comments