advertise with us

ADVERTISE HERE

KUELEKEA MAPINDUZI CUP NABI AONDOKA YANGA KIMYA KIMYA

 Wakati klabu ya Yanga ikiendelea na mazoezi kuelekea michezo ya kombe la mapinduzi  Zanzibar Kocha mkuu wa klabu hiyo  Nesreddine Nabi ameondoka kimya kimya kuelekea ulaya kwa mapumziko ya siku 10.Kocha huyo raia wa Tunisia ameiambia amospoti kwamba anakwenda kitazama familia yake iliyopo Ubelgiji na atarejea baada ya siku 10.

“Ni muda sijaonana na familia yangu, watu wangu wengi walirudi makwao ila mimi nilibaki kwa ajili ya majukumu mengi ya klabu, nimeona nitumie muda huu kama siku 10 kukaa na familia, kabla ya kurejea baadaye kwa majukumu zaidi,” alisema Nabi na kuongeza;

“Sitaweza kuwa sehemu ya kikosi cha michuano ya Kombe la Mapinduzi. Nilitamani kuwa hapa lakini haitakuwa sawa, kwani kama nsiipoondoka sasa, sitaweza tena. Kumbuka natakiwa kuwa hapa kwa ajili ya ligi itakavyoendelea.”

Klabu ya Yanga itaongozwa na kocha msaidizi kwenye michuano hiyo iliyokwisha anza tangu tarehe 2 na Yanga wataondoka leo jion.Post a Comment

0 Comments