KIIZA AIMALIZA SIMBA NA KUONDOSHWA DAKIKA YA 90

 MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ ametokea benchi kuifungia bao pekee Kagera Sugar ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi Simba 


katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Kiiza aliingia dakika 56 kuchukua nafasi ya Ally Ramadhani na akafunga bao hilo dakika ya 70 akimalizia pasi nzuri ya Ally Nassor ‘Ufudu’, kabla ya Mganda huyo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Kagera Sugar inafikisha pointi 17 na kupanda hadi nafasi ya nane, wakati Simba inabaki na pointi zake 25 katika nafasi ya pili, ikizidiwa pointi 10 na vinara, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi 13 za msimu

Post a Comment

0 Comments