WAkati timu zingine kama Simba Yanga Azam na Namungo zikiendelea na michuano ya Mapinduzi Cup inayochezwa Zanzibar upande wa pili vilabu mbalimbali vimeendelea kujinoa na michezo ya ligi kuu
Geita Gold na wao ni moja ya timu hizo ikijiimarisha kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma utakaopigwa January 15 kwenye dimba la Jamhuri daodoma na tarehe 22 watakuwa mjini mara dimba la Karume kumbenyana na Biashara United kisha kurejea nyumbani kwa mchezo wa FA.
Geita imeanza vibaya msimu huu kwa kucheza michezo 11 ikiwa na pointi 12 na kushika nafasi ya 9 ,inatakiwa kuongeza juhudi zaidi ili kuepuka kushuka daraja mwishoni mwa msimu na kwa kufanya hivyo kikosi hicho kimemsajili beki wa kushoto kutokea Yanga Adeyun Salehe, mshambuliaji Ditram Nchimbi kutoka Yanga na Golikipa Aaron Kalambo kutoka Prisons .
Hizi hapa ni baadhi picha za kikosi hicho kikifanya mazoezi
0 Comments