Hatimaye kikosi cha Yanga kimefanikiwa kuondoka mchana wa leo kuelekea Zanzibar kushiriki michuano ya Mapinduzi Cup yaliyoanza tangu january 02 visiwani humo.
Hapo awali kikosi hicho na viongozi wake walijiweka mafichoni kujiandaa na michuano hiyo na hakukuwa na picha wala habari juu ya kusafiri au kuonekana wakifanya mazoezi. Mbali na kikosi hicho kuondoka ila kitawakosa nyota wake 6 wa kikosi cha kwanza akiwemo Fiston Mayele ,Khalid Aucho,Saido Ntabayonkiza,Diara,Mukoko Tonombe na Jesus Moroko.
Kocha Nabi amesafiri kuelekea nchini Ubelgiji kwa mapumziko huku CAEDRIC KAZE akiwa nchini Burundi.Kocha mwinyi Zahera atakiongoza kikosi hicho mjini Zanzibar.
hizi ni baadhi ya picha za wachezaji
0 Comments