advertise with us

ADVERTISE HERE

AHMED ALLY ATAWEZANA NA HAJI MANARA ? AWAVAA TENA YANGA

 Msemaji Mpya wa Simba Ahmed Ally ni kama anawachokoza mashabiki wa Yanga baada ya kutoa kauli yenye utata mara Simba walipotambulisha jezi mpya za Mapinduzi CupKupitia Instagram Ahmed Ally aliandika

 Yessss Mabingwa wa Nchi tumezindua Jezi mpya kwa ajili ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi na Ile ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports....Jezi zinapatikana kwenye maduka yote ya @vunjabeiSisi sio kauka nikuvae tunavaaa Jezi mpya tena Jezi Bora kila mashindano...

Kauli yake hiyo imetafsiriwa kama ni dongo kwa mashabiki wa Yanga kwani wao  watatumia jezi zao za ligi kuu kwenye michuano hiyo. Mpaka sasa hakuna msemaji wa Yanga kati ya Bumbuli na Manara waliojitokeza kutoa majibu ya maneno anayoyatoa Ahmed Ally huku kauli ya kwanza aliandika 

Safari kuelekea Zanzibar 🦁🦁Safar kwenda kuchukua Kombe la Mapinduzi
Yess ni rahisi na inawezekana tupo tayari.Tunafahamu wengine hili ndo Kombe lao pekee la kujivunia hivyo tunalichukua Ili tuwakumbushe kuwa sisi ni Wakubwa kwao.Saa 8:20 Insha Allah, Nitakua Forodhani na baadae saa 11:15 nitahudhuria mazoezi ya kwanza ya timu katika Uwanja wa Mao tse Tung🦁🦁

Swali ni je Msemaji huyo atavumilia kejeri na karaha za haji manara? Hii ni ligi nje ya uwanja mashabiki wanataka kujua nani mbabe wa maneno kati yao.


Post a Comment

0 Comments