MESSI AMTUMIA SALAMU RONALDO BAADA YA KUMPOTEZA PELE

 Rekodi zimewekwa ili kuvunjwa na msemo huu unajidhihirisha hivi sasa baada ya Mchezaji Bora wa Dunia kwa mwaka 2021 Lionel Messi kufanikisha kuvunja rekodi ya Dunia na kuwa mchezaji namba mbili duniani mwenye mabao mengi.

 Rekodi hiyo inashikiliwa na Josep Biccan mwenye mabao 805 akifuatiwa na Cristiano Ronaldo mwenye mabao 801 nafasi ya tatu ikishikiliwa na Romario mwenye mabao 772 huku nafasi ya nne ikishilikiwa na Lionel Messi 758 akivunja rekodi ya Pele mwenye mabao  akiwa na mabao 757 akishika nafasi ya 5.

Messi ameweka rekodi hiyo baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Club Brugge kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya kwenye ushindi wa mabao 4-1 huku mengine yakiwekwa kimiani na kiliani mbappe.

Lionel Messi ameendelea kuvunja na kuweka rekodi mbalimbali duniani na ni wiki chache tu aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza duniani kubeba tuzo ya Ballon D or kwa mara ya saba.Swali n je ataweza kumfikia Cristiano Ronaldo mwenye mabao 801? hizo ni salam kwa msimu wa 2020/21

Jambo kubwa zaidi kwa Lionel Messi kwa Pele ni kuvunja rekodi tatu kubwa za mchezaji huyo wa zamani ikiwemo

1.magoli mengi ndani ya klabu moja 

🇦🇷 Leo Messi – 672

🇧🇷 Pelé – 643

2.Mchezaji wa America Kusini mwenye mabao mengi

🇦🇷 Leo Messi – 80

🇧🇷 Pelé – 77

3.Mchezaji wa America Kusini mwenye mabao mengi duniani

🇦🇷 Leo Messi – 758

🇧🇷 Pelé – 757

Post a Comment

0 Comments