BETI NASI UTAJIRIKE

MBAPPE AMVUNJIA HESHIMA LIONEL MESSI

Mchezaji wa PSG Kylian Mbappe ameweka rekodi mpya kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Club Brugge kwenye mchezo wa mwisho wa makundi.

 Mabao haya yanamfanya Mbappe kufikisha mabao 30 akiwa na miaka 22 na siku 252 huku rekodi ya awali ilikuwa inashikiliwa na mchezaji mwenza Lionel Messi aliyefunga mabao 30 akiwa na miaka 23. Mbape amefikia rekodi hiyo baada ya kucheza michezo 9 akiwa na Monaco na kufunga mabao 6 huku akicheza michezo 42 na kufunga mabao 25.

Mbappe ndiye mchezaji pekee aliyeifikia rekodi hiyo ya Lionel Messi aliyoiweka mwaka 2009 na mchezaji huyo amevunja rekodi hiyo mbele ya Lionel Messi wanayekipiga klabu moja na kitendo hicho kutafsiriwa kuwa ni utovu wa nidhamu mbele ya Messi mwenye rekodi mbalimbali kwenye soka. 


Post a Comment

0 Comments