KUELEKA DABI: SIMBA WAKO TAYARI KUSHUKA DARAJA

 Kuelekea Mchezo wa ligi kuu NBC kati yaa watani wa jadi  Simba na Yanga utakaopigwa Disemba 11 dimba la mkapa ,tayari figisu zimeshika kasi na kuwafanya mashabiki wa Simba kucharuka zaidi na kutangaza wako tayari kushuka daraja au kulipa faini ya milioni tatu kila mechi.


hayo yote yameibuka baada ya kampuni ya GSM inayoidhamini klabu ya Yanga ,Namungo na Coastal Union kuingia mkataba wenye thamani ya bilioni mbili na TFF kama mdhamini mwenza wa ligi ya NBC. Suala hilo lilizua tafrani kwa mashabiki wa Simba walipoelezwa na vyanzo visivyo rasmi kuwa watalazimika kuvaa jezi yenye nembo ya GSM kwenye mchezo huo wa Disemba 11.

Na kunataarifa zisizo rasmi zinazosema kama Simba hawatovaa jezi zenye nembo hiyo basi adhabu yake ni kushushwa daraja au kulipa faini ya milioni 3 kwa kila mechi wanayocheza bila nembo hiyo

Baadhi ya mashabiki walinukuliwa wakisema " Tupo tayari kushuka daraja lakini hatuwezi kuvaa jezi zenye nembo ya GSM,wale wanataka kutafuta umaarufu kupitia Simba lakini pia tunajua wanawadhamini9 Yanga na wamewekeza pale na hiyo ni njia ya kutudhoofisha,na kama watataka hizo milioni 3 tupo tayari kutoa"

Mbali na maneno mengi ya mitandaoni Uongozi wa Simba haujafunguka kusema lolote kuelekea mchezo huo hususani madai hayo yanayotolewa.

Amospoti inawakumbusha mashabiki wa Simba kuwa kipindi hiki ni cha kucharulana watani wa jadi hivyo si kila taarifa ni rasmi

Post a Comment

2 Comments

  1. Simba wako sahihi kulingana na kanuni za ligi zinavosema

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni wakati sasa wa Bodi ya ligi na TFF kutoa ufafanuzi ili kuondoa hii sintofahamu

      Delete