BETI NASI UTAJIRIKE

KIFAA CHA YANGA CHATUA GEITA GOLD

 Hatimaye mshambuliaji wa zamani wa Yanga Ditram Nchimbi ametua rasmi GEITA Gold. Ditram aliachana na Yanga baada ya mkataba wake na mabingwa hao wa kihistoria kumalizika. 

Ditram ni moja ya mastraika waliozitumikia klabu mbalimbali za ligi kuu ikiwamo majimaji, njombe mji, mbeya city, Polisi Tanzania, Yanga na sasa GEITA gold. Kupitia ukurasa rasmi wa GEITA gold wamenukuliwa wakisema

"Geita Gold FC FC tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na Mshambuliaji, Ditram Adrian Nchimbi 'DUMA' (@ditram_nchimbi_02 ), tuliyemsajili kutoka Yanga SC ya Jijini Dar es Salaam

Nchimbi  ni miongoni mwa washambuliaji wazuri, akiwa amevitumikia vilabu kadhaa hapa nchini kama vile Majimaji, Mbeya City, Njombe Mji pamoja na Mwadui pia akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa vipindi tofauti tofauti, anakuja kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji kwenye timu yetu.

Huo unakuwa usajili wetu wa tatu sasa kuelekea dirisha dogo la usajili, tukiwa na nia ya dhati kabisa ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) pamoja na Ligi Kuu (NBCPL"

Post a Comment

0 Comments