Kikosi cha Wachezaji wa klabu ya azam fc kimefanikiwa kufika salama nchini misri kukabiliana na wapinzani wao Pyramids kwenye kombe la shirikisho.
Mchezo wa kwanza ulipigwa dimba la Chamazi na matokeo yalikuwa ni 0-0 .Mchezo huu wa pili ni muhimu sana kwa timu zote mbili kwani mshindi wa mchezo huo ataingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.
Azam wanapaswa kutafuta sare yoyote ya kufungana au kushinda mechi hiyo ili waweze kusonga mbele huku Pyramids wakitakiwa kushinda mchezo huo kwa namna yoyote.
Nimekuwekea video fupi ya msafara mzima wa azam kuanzia kambini chamazi kuelekea Misri.tazama video hapa chini.
0 Comments