MZUNGU AWABULUZA MANARA NA MASAU BWIRE TFF AWARDS

 Nick Leonard maarufu kama Bongo Zozo ameibuka ndiye msemaji bora wa tuzo za TFF kwa msimu wa 2020/21. Bongo zozo anakuwa mhamasishaji wa kwanza kutwaa tuzo hizo tangu kuanzishwa kwake akiwabwaga chini Msemaji wa Yanga Haji Manara na Masau Bwire wa Ruvu Shooting.


Baadhi ya Mashabiki wamehoji ni kigezo gani kimetumika kwa Mhamasishaji huyo kutwaa tuzo hizo. Kwanza ifahamike kuwa Bongo zozo ni mmoja wa wahamasishaji wakubwa kwa timu ya Taifa Taifa Stars na mara zote amekuwa akishiriki kutazama mechi za Taifa Stars ,kusafiri na timu nchi mbali mbali na itakumbukwa hata michuano ya AFCON iliyopigwa nchini Cameroon alishiriki.

Mbali na michuano hiyo lakini pia amekuwa akiitangaza Tanzania hasa kwa nchi za ulaya na mara zote amekuwa akienda uwanjani na kushawishi mashabiki wafuatilie soka la Tanzania ,hicho ni kigezo tosha kinachomfanya atwae tuzo hiyo hasa ikizingatiwa ni mgeni na anasapoti maendeleo ya soka letu

Post a Comment

0 Comments