FEI TOTO AWA GUMZO TUZO ZA TFF AWARDS

 Kiungo wa Yanga Feisal Salum amegeuka kuwa stori mtandaoni baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Azam Sports Federation Cup akiwamwaga Luis Miquisonne aliyekuwa mchezaji wa Simba. Mbali na tuzo hiyo lakini pia aliingia kwenye kikosi bora cha msimu wa ligi kuu Tanzania Bara akiungana na wachezaji wenzake kutoka Yanga Mukoko Tonombe na Dickson Job.

Feisal alizua mjadala zaidi baada ya moja ya goli lake kuingia kwenye kinyang'anyiro cha goli bora la msimu tuzo ambayo ilikwenda kwa Lambert Sabiyanka wa Tanzania Prisons . Laurent Lusajo aliibuka mfungaji bora wa msimu kwa upande wa Azam Sport Federation Cup.

Ramadhani Kayoko aliibuka ndiye mwamuzi bora wa ligi kuu Tanzania na Frank Komba akiibuka Mwamuzi bora saidizi. kwa upande wa mchezaji chipukizi tuzo ilikwenda kwa Abdul Seleman. King Abdallah Mputa Kibaden nguli wa soka la Tanzania aliibuka ndiye gwiji wa soka letu

Post a Comment

0 Comments