UBINGWA UPO YANGA NI SUALA LA MUDA TU

 Mashabiki wa klabu ya Yanga wameingia kwenye hofu kubwa ya kuukosa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya timu hiyo kushindwa kuonyesha makali na kupoteza mechi dhidi ya Azam Fc mchezo uliopigwa hapo hana dimba la Benjamin Mkapa.

Yanga walitegemea kushinda mchezo huo ili waweze kurudi kileleni lakini mambo hayakwenda kama walivyotarajiwa baada ya Prince Dube kutandika shuti hatari lililomshinda farouk Shikhalo na kuzama nyavuni dakika ya 86 ya mchezo huo. mtanange huo mkali ulimalizika kwa timu Azam kushinda bao 1-0

Matokeo hayo Yanaifanya Yanga ibakie nafasi ya 2 ikiwa na pointi 57 huku wapinzani wao Simba wakiwa na pointi 58 wakiongoza ligi na pia wanamechi tatu za viporo.Endapo Simba atashinda mechi hizo zote basi Yanga watazidi kuwa na wakati mgumu zaidi kutwaa taji hilo.

Shabiki Kindaki wa Yanga anayefahamika kama Hassan Yangayanga amenukuliwa akisema "Ubingwa bado haujapoteza kwani tunamechi tisa mkononi na kama tukishinda zote basi ubingwa ni wakwetu ,Simba hawezi kushinda mechi zote tunajua atapoteza tu na sisi ndio tutakwenda kutwaa taji hilo"

Post a Comment

0 Comments