MANCHESTER CITY WAMESHAANZA KUKUSANYA MAKOMBE MSIMU HUU

Klabu ya Manchester City imeendelea kuwa tishio kwa soka la Uingereza baada ya kutwaa kombe la Ligi kwa mara ya nne mfululizo huku timu hiyo ikiibuka bingwa mara 5 kwenye misimu 6 ya hivi karibuni .
Manchester City  waliibuka na ushindi wa bao 1 dhidi ya Tottenham . Fainali hiyo ilipigwa dimba la wembley na vijana wa Gyardiola walitwaa kombe hilo kwa bao murua lililowekwa kimiani na Aymeir Laporte dakika ya 82 aipokea pasi safi kutoka kwa Kelvin De bruyne.

Mpaka sasa Manchester City ina kikombe kimoja huku ikiwa na matumaini makubwa ya kutwaa kombe la ligi kuu Uingereza akiwa na pointi 77 na anahitaji kushinda mechi mbili tu aweze kutangazwa Bingwa.mchezaji Mahrez aliibuka mchezaji bora wa mechi na alitwaa tuzo

Kwa upande wa kimataifa wamefanikiwa kuingia nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya wakiwa na mategemeo ya kuvuka hatua hiyo na kuingia fainali.Mancity wamepangwa na PSG na mchezo wao.Timu hii imekuwa moto mkali kwa ulaya na Uingereza tangu ilipoanza kunolewa na Pep Guardiola.


Post a Comment

0 Comments