BETI NASI UTAJIRIKE

MWAMBUSI AFUNGUKA KUREJEA YANGA

Aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi cha klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa kwa sasa yupo fiti kurejea ndani ya kikosi hicho, hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa jino.

Mwezi mmoja uliopita, Mwambusi alitangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya kikosi cha klabu ya Yanga, hii ni baada ya kushauriwa na daktari kutokana na kuwa na matatizo hayo ya kiafya ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Nizar Khalfan.

Akizungumzia maendeleo yake Mwambusi amesema: “Tayari nimepata matibabu ya jino, na ni kama wiki mbili zimepita tangu nifanyiwe upasuaji, naendelea vizuri na sina maumivu kama ilivyokuwa mwanzo.
“Wanamichezo waniombee nipone ili niweze kurejea katika majukumu yangu kama ilivyokuwa awali, na endapo nitakuwa sawa basi naweza kurejea Yanga”

Post a Comment

0 Comments