BETI NASI UTAJIRIKE

MBAPPE NA HALAAND WATAKUWA BORA ZAIDI YA MESSI NA RONALDO? (SEHEMU YA 1)

 Baada ya Messi na Ronaldo ni nani atakayefuata kulitawala soka la dunia hii? Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiulizana swali hili na ilifia mahali kila mtu aliamini hakuna mtu wa kuvunja au kufikia rekodi zao. 


Binafsi naamini warithi wa magwiji hao wamekwishapatikana na kutoka msimu huu wa 2020/21 basi jina la Haaland na Mbappe yatatamkwa bila kukoma kutokana na umahili wao wanaouonyesha ndani ya uwanja. 

Mbappe mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akionyesha uwezo mkubwa sana anapoitumikia timu yake ya taifa pamoja na PSG na mpaka anatimiza umri huo amekwishafunga mabao 138 ndani ya klabu ya PSG na Monaco.

Haaland naye hayuko nyuma kwani kwani ya umri wa maika 20 ameshafunga mabao 79 kwenye vilabu mbalimbali alivyovitumikia. Nyota huyu anaonekana mdogo kwa umri lakini umakini wake wa kuziumania nyavu umefanya timu pinzani kumhofia kama zinacheza na mchezaji mkongwe.

1. MBAPPE VS HALAAND MWAKA 2020

Mbali na kwamba mwaka 2020 ulikuwa na changamoto za janga la Corona lakini hiyo haikuzuia nyota hao kungaa. Halaand aliyetua Borrusia Dortmund alikuwa mwenye makali zaidi baada ya kucheza michezo 42 akifunga mabao 41 huku akitengeneza mengine 7. Ni mwaka huo huo ambao nyota huyo alimaliza nafasi ya pili ufungaji bora michuano ya UEFA akiwa na mabao 10. 

Mbappe na yeye alikuwa na msimu mzuri baada ya kufunga mabao 30 kwenye michezo 44 aliyocheza huku akitengeneza mabao 13 kwa timu yake ya PSG. Mbappe amekuwa msaada mkubwa kwa klabu yake na tumeshuhudia uwezo wake naamini mwaka 2021 kati ya yeye au Haaland basi wataifanya dunia ya soka kuwa yakipekee sana.

itaendelea


Post a Comment

0 Comments