Klabu ya Simba imetangaza zabuni ya jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2020-21. Ni kama Simba imeamua kubadili gia na kuachana na kampuni ya Iliyokuwa ikisambaza jezi za klabu hiyo ya Uhl Sport.
Kwa msimu wa 2020-21 mashabiki wa klabu ya Simba walikuwa wanalalamika ukosefu wa ubunifu kwa jezi zao zilizokuwa zikifanana sana na zile za msimu wa 2018-19. Mbali na hayo jezi za watani wao Yanga zilikamata soko na ziliuzwa kila mahali ukilinganishwa na jezi za Simba
Baada ya lawama nyingi kwa uongozi Simba wanataka kampuni mpya zenye ubunifu na uzoefu zaidi katika biashara ya nguo za kimichezo hivyo wametangaza zabuni kwa yeyote mwenye uwezo wa Kusambaza jezi mpya. Hii ni barua ya simba kwenda kwa makampuni yenye uwezo wa Kusambaza jezi hizo
Baadhi ya wadau wanaamini makampuni kama Adidas, Nike na Puma yanaweza kuomba tenda hiyo na kufanya klabu hiyo kuwa na mbunifu mwenye Hadhi zaidi.
Mbali na makampuni ya nje lakini makampuni kama Vunja bei watengenezaji wa jezi za Lipuli msimu wa 2019/20 na ile ya Bongo iliyotengeneza jezi za Lipuli msimu wa 2018-19 zinaweza kuomba.
GSM ambao pia ni wadhamini wa klabu ya Yanga na wasambazaji rasmi wa jezi za klabu hiyo wanaweza kuomba nafasi ya Kusambaza jezi za Simba kwani tumeshuhudia thamani walivyoipandisha jezi ya Yanga na kufanya iwe jezi ya thamani kwa msimu wa 2020-21.
0 Comments