Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, amedokeza kuwa nafasi ya yeye kuondoka Paris St-Germain itategemea ridhaa ya wazazi wake. (Copa 90, via Sun on Sunday)
Juventus wana matumaini kuwa Manchester United watamruhusu kiungo wa kati Paul Pogba, kurejea Turin kwa mkopo mwezi ujao. (Sunday Mirror)
United tayari wamekataa mpango wa kubadilishana na Juve wakiwahusisha winga Douglas Costa, 30, na kiungo wa kati wa Barcelona Miralem Pjanic,30, ili kumnasa Pogba. (Calciomercato)
Baba wa Erling Braut Haaland- mchezaji wa zamani wa Leeds Alf-Inge- amesema kuwa mshambuliaji wa Norway ana furaha sana akiwa Borussia Dortmund hivi sasa, lakini anaweza kuendelea mbele siku za usoni. (Tuttosport - in Italian)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta hajamkataa mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil anayechezea kikosi cha washika bunduki kabla ya mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 32 kumalizika msimu huu. (Star on Sunday)
Wolverhampton Wanderers walishindwa uhamisho wa pauni milioni 19 kwa beki wa kushoto wa Manchester City Oleksandr Zinchenko msimu huu, lakini wako tayari kutoa zabuni nyingine kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine katika dirisha la uhamisho la Januari. (Star on Sunday)
Kocha wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal amesema kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 23, hakufanya "chaguo nzuri" kujiunga na Old Trafford. (Ziggo Sport - in Dutch)
Chelsea wanajitahidi kutafuta wanunuzi wa kipa Kepa Arrizabalaga, 26, beki wa kushoto Mhispania Marcos Alonso, 29, na mlinzi wa Kidenmark Andreas Christensen, 24, ambao wote watapatikana mwezi Januari. (Sunday Express)
Mwenyekiti wa Tottenham Hotspur, Daniel Levy yuko tayari kuidhinisha mkataba wa mkopo wa miezi 18 kwa kiungo wa England mwenye umri wa miaka 24 Dele Alli, ambaye anataka kuondoka klabuni hapo mwezi Januari ikielezwa kuna uwezekano anaelekea Paris St-Germain. (90min)
Wolves wanafikiria kumchukua kiungo wa kati wa Mainz Marlon Roos-Trujillo, 17, ambaye amewakilisha Ujerumani kwa wachezaji wa chini ya umri wa miaka 19. (Bild - in German)
West Bromwich Albion wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 anayekipiga Newcastle United Dwight Gayle, ambaye mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Birmingham Live)
Arsenal wamepanga kumfanya mlinzi wa Ufaransa 19 William Saliba mwenye umri wa miaka 19 apatikane mwezi Januari, akiwa na mashaka juu ya utayari kwa Soka la Primia . (Football London)
Kocha wa Middlesbrough Neil Warnock anamtaka winga wa Uingereza Duncan Watmore mwenye umri wa miaka 26 kutia saini mkataba mpya wakati vilabu vingine vikimhitaji. (Sun on Sunday)
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameghairi chakula cha mchana wakati wa sikukuu ya Krisimasi kwa sababu ya hofu ya Covid-19. (Sunday Mirror)
0 Comments