Simba waendeleza ubabe ligi kuu

 Klabu ya Simba imeendelea ubabe kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City. Mchezo huo ulichezwa katika dimba la Sokoine na shukrani za kipekee zimwendee John Raphael Bocco aliyefunga bao hilo dakika ya 29 akipokea pasi kutoka kwa Clatous Chota Chama.

Kwa matokeo hayo Simba imesogea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 29 kwenye michezo 12 iliyokwisha kuicheza.John Bocco anasalia kuwa namba moja kwenye orodha ya wafungaji bora ligi kuu akiwa na mabao 8 huku Clatous Chama akiwa top assist kwa msimu huu baada ya kufanya hivyo mara 7

Post a Comment

0 Comments