NANI KUSONGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA ?

Chama cha soka Ulaya kinachosimamia Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa UEFA kimemaliza mchakato mzima wa kuzipangia timu 16 kucheza htua ya mtoano kwenye michuano hiyo . Habari kubwa ni mechi ambayo imekuwa gumzo ni ile ya PSG dhidi ya Barcelona .

Mara ya mwisho kwa kwa timu hizo kukutana Barcelona aliibuka na ushindi wa mabao 6-1 kwenye mchezo wa pili wa raundi ya 16 uliopigwa Machi 6 mwaka 2017 dimba la Nou Camp huku mchezo wa awali PSG walikuwa wameshinda mabao 4-0.

Kwenye  mchezo ule Neymar alikuwa nyota wa Barcelona na alifunga mabaomawili na kuibuka nyota wa mchezo huo. Kwa sasa Neymar ni mchezaji wa PSG na swali kubwa ni moja tu ataweza kuiadhibu timu yake ya zamani?

Mechi Zingine ni ule wa Atletico Madrid dhidi ya Chelsea ,RB Leipzig dhidi ya Liverpool na Bayern Munich dhidi ya Lazio.Hii hapa ni ratiba kamili.Post a Comment

0 Comments