NADO AENDELEA KUWASHA MOTO AZAM IKISHIKWA SHATI NA NAMUNGO

Azam FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Namungo FC ya Ruangwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 

Mara mbili winga Iddi Suleiman ‘Nado’ aliitanguza Azam FC dakika ya 19 na 74, lakini mar azote Namungo FC ikasawazisha kupitia kwa beki Edward Charles Manyama dakika ya 25 na mshambuliaji Mghana, Stephen Sey dakika ya 90 na ushei.

Na kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 15 na inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 29 za mechi 13 na Yanga SC wenye pointi 37 za mechi 15 pia. 

Namungo wamefikisha pointi 17 baada ya kucheza michezo 13 na kupanda mpaka nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi  wenye timu 18 ambayo mwishoni mwa msimu wa 2020/21 timu mbili zitashuka daraja na timu mbili zitacheza michezo ya mtoano na timu za daraja la kwanza 


Post a Comment

0 Comments