MAMBO MAZURI YAANZA KUNOGA SIMBA

Klabu ya Simba ilitangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Swedi Mkwabi.


Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Boniface Lihamwike aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam kuwa uchaguzi huo umepangwa kufanyika Februari 7, 2021
Mkwabi alijiuzulu nafasi hiyo mwaka juzi kwa madai ya kutingwa na shughuli zake binafsi na nafasi yake kukaimiwa na mwanachama wa siku nyingi wa Simba, Mwina Kaduguda

"Uchaguzi utakuwa mdogo wa kuziba nafasi moja ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Mkwabi kwa hiyo inahitajika kuziba nafasi yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu kuhakikisha anapatika kiongozi aliyechaguliwa na wanachama"

"Uchaguzi utafanyika Februari 7/2021, nawaahidi wapenzi na mashabiki wa Simba utakuwa huru na wa haki, tutasimamia kanuni zote kwa kuzingatia Katiba ya Simba na za Shirikisho la Soka (TFF)," alisema Lihamwike

Naye Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Steven Ali alisema mchakato huo ulianza jana kwa wanachama wanaohitaji kuwania nafasi fomu zinaanza kutolewa kuanzia leo hadi Desemba 23

"Kwa siku hizo Desemba 14-hadi 23 fomu zitatolewa na kurudishwa na kuanzia Desemba 27 hadi 28 kamati itakuwa kwenye majukumu ya ndani kufanya usahili kwa wanaowania," alisema Ali.

Pia alisema Desemba 29 hadi 30 kamati hiyo itaweka hadharani majina yaliyopitishwa na Januari 2/2021 ni siku ya kupokea na kupitia mapingamizi yaliyokidhi vigezo kwa wagombea.

"Januari 3/2021 ni siku ya kutoa maamuzi na siku itakayofuata kutangaza majina ya wagombea watakaopitishwa na kamati wakati Februari 5 hadi 6 /2021 kipindi cha kampeni na siku itakayofuatia ni uchaguzi" alisema

Ali alisema gharama za kuchukua fomu ni Sh 30,000 na vigezo vya mgombea kama inavyoeleza kwenye Katiba ya Simba kwenye ibara ya 27 lazima awe mwanachama hai na elimu ya stashahada inayotambulika na Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)

Post a Comment

0 Comments