Maajabu ya leo ni klabu ya Schalke 04 ambayo imecheza michezo 11 ikipata sare 4 na kufungwa michezo 7 huku ikiwa haijashinda mchezo wowote tangu mwezi July 2020. Klabu hii imefungwa mabao mengi zaidi huku ndani ya bundesliga ilifungwa mabao 33 kwenye michezo 11 na kufunga mabao 8 tu.
Klabu hiyo ilifilisika na kupelekea baadhi ya wachezaji na viongozi wa juu kuondoka kutokana na deni la paundi milioni 200 wanalodaiwa huku pia kukitegemewa deni hilo kuongezeka maradufu. timu hiyo haijashinda mchezo wowote kwenye mechi 25 ilizocheza na kuifanya izidi kupotea kwenye ramani ya soka la ushindani ulaya.
Klabu hiyo inashika mkia kwenye msimamo wa Bundesliga na gakuna dalili za kuiokoa klabu hiyo kutoshuka daraja kwa msimu wa 2020/21
0 Comments