AZAM WAIPIGA BAO YANGA KWA MOZIZI

Klabu ya Azam Fc imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili mshambuliaji Mozizi aliyekuwa anakipiga Lupopo ya DRC Congo Awali mshambuliaji huyo alihusishwa kutakiwa na Yanga lakini dau lilikuwa dogo.

Azam Fc kupitia mitandao ya kijamii waliweza Taarifa za nyota huyo kuwasili na walinukuliwa wakisema 

"Mozizi aliyekuwa akicheza Lupopo ya huko, amewasili nchini  leo mchana, tayari kukamilisha taratibu za kujiunga na Azam FC, na hii ni endapo atafuzu vipimo vya afya atakavyofanyiwa kesho Jumatano.

Mshambuliaji huyo kinara, atakapofuzu vipimo vya afya, anatarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Azam FC na kuziba nafasi ya Thierry Akono, tuliyemuuza Negeri Sembilan ya Malaysia.

Mbali na vipimo vya kawaida vya afya atakavyofanyiwa, pia atafanyiwa kipimo maalumu cha kujua utimamu wa mwili wake.

Habari zaidi zitawajia kesho Jumatano, tunakuomba endelea kuwa nasi kwenye mitandao yetu ya kijamii."

Post a Comment

0 Comments