ANTONY JOSHUA AWEKA REKODI MPYA DUNIANI

Anthony Joshua (31) usiku wa jana ametetea mataji yake ya WBA, WBO, IBF and IBO baada ya kumshinda Mbulgaria, Kubrat Pulev kwa Knockout (KO) raundi ya tisa katika pambano la uzito wa juu mbele ya mashabiki 1,000 Uwanja wa Wembley Jijini London.

Baada ya kushinda pambano la 25 kati ya 26 aliyocheza, akiwa amepigwa moja tu – sasa Joshua anaweza kupanda ulingoni kupigana na Muingereza mwenzake, bingwa wa WBC Tyson Fury katika pambano la kuunganisha mataji.

Joshua alikuwa anapigana kwa mara ya kwanza tangu arejeshe mataji yake hayo Saudi Arabia Desemba mwaka jana akimshinda Mmexico, Andy Ruiz Jr kulipa kisasi cha Juni 2019, wakati, Pulev (39), aliyepoteza pambano la pili jana kati ya 29 aliyocheza hadi sasa, linguine akipigwa na Wladimir Klitschko mwaka 2014

Post a Comment

0 Comments