YANGA WAZIDI KUMKOMALIA BENARD MORRISON KUSALIA KLABUNI


Klabu ya Yanga imezuia kibali cha kufanya kazi nchini winga Bernard Morrison wakimtambua mchezaji huyo kuwa mali yao
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Morrison ana mkataba halali na Yanga hata Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ililitambua hilo licha ya kudai kuwa mkataba huo una mapungufu
Akihojiwa na Wasafi Radio mapema leo, Bumbuli amesema walipokea barua kutoka wa Afisa wa Idara ya Uhamiaji akiwataka warudishe kibali cha kazi cha Morrison
"Tumepokea barua kutoka kwa Afisa wa idara ya Uhamiaji akitutaka turudishe kibari cha Morrison haraka sana. Ni jambo lililotushangaza kwani tumewahi kuachana na wachezaji wengi wa kigeni lakini hatukuwahi kuandikiwa barua na aina hii, tumejiuliza kuna jambo gani nyuma ya barua hii?," alihoji Bumbuli
"Kama klabu tumeweka wazi msimamo wetu kuwa tunamtambua Morrison kama mchezaji wetu halali hivyo kibali chake tutaendelea kubaki nacho mpaka pale shauri lake litakapopatiwa ufumbuzi. Jana tumewasilisha rufaa yetu Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), tunasubiri maamuzi"
Morrison hataweza kuitumikia Simba mpaka pale Yanga ambayo ndiyo iliyomleta nchini mara ya kwanza na kumkatia kibali cha kufanya kazi, itakaporudisha kibali hicho Serikalini
Inaelezwa hata klabu ya Simba imegoma kutoa kibali cha aliyekuwa Mtendaji wao Mkuu Senzo Mazingisa ambaye aliikacha timu hiyo na kujiunga na Yanga

Post a Comment

0 Comments