YANGA WATANGAZA VITA NJE YA UWANJA NA SIMBA


Mahabiki wa soka nchini walizoea vita ya Simba na Yanga ni zile dakika 90 za uwanjani lakini kwa sasa mambo ni tofauti kwani viongozi wa klabu hizo wametutangazia kuwa vita hivyo vitapigwa nje ya uwanja na baadaye uwanjani.

Kitenzo cha Simba kumsajili Morrison na baadaye Yanga kumsajili Senzo Mbatha ni ishara kuwa timu hizo zimeingia kwenye vita kali zaidi.


Habari kutoka ndani ya klabu ya  Yanga zinasema kuwa kazi ndiyo kwanza imeanza na taratibu watajibu mapigo makali kwa Simba siku chache zijazo.Mmoja wa wadau wa klabu hiyo amenukuliwa akisema 

"Ni kweli kuna picha ambayo imeonekana na alikuwa ni Senzo lakini siwezi kuzungumzia alikuwa anafanya nini.Ukitaka kuchukua vifaranga anza na mama kwanza kisha wengine watafuata ndivyo ilivyo hivyo tumeanza na mama kisha vifaranga vitafuata.

"Tumekuwa na utaratibu wa kuchukua wachezaji wetu kutoka kwetu na wao pia wamekuwa wakichukua wachezaji kwetu, walimchukua Niyonzima, Gadiel ila hatujasema kitu nasi pia tulikuwa tunachukua wachezaji wao.

"Lakini kuna watu ambao wamekuwa na ukorofi na wanavuruga mpira, sisi tuliokuwa tumekaa mafichoni sasa tumeamka ili tuonyeshane nani atalia ama atacheka," ameeleza mtoa taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments