BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WATANGAZA TAREHE RASMI YA KOCHA WAO KUWASILI


Msemaji na Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu, waendelee kuiunga mkono timu yao kwani wamedhamiria kuwapa furaha msimu ujao
Aidha Nugaz amesema wanasubiri kuwasili kwa Kocha Mkuu, hivyo atatangazwa wakati wowote baada ya kuwasili
"Kikubwa tuendelee kuiombea dua timu yetu kuelekea msimu mpya na Insha Allah muda wowote Mwalimu atatua na tutamtangaza"
"Mashabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga tuendelee kushikamana na kuwa na Subra naamini tutakwenda Kuwa na kikosi Bora chenye mvuto, uwezo na cha ushindani," alisema Nugaz
Baada ya kufanyika mchujo mkali kutoka majina ya makocha 64 mpaka majina matatu, Cedric Kaze raia wa Burundi ndiye anayetajwa kuibuka kidedea kumrithi Luc Eymael
Jina hili linaweza kuwa geni kwa mashabiki wengi, lakini ni kocha mwenye CV ya kutisha! amefanya kazi barani Ulaya kwa muda mrefu

Kaze amewahi kufanya kazi kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana ya Ujerumani mwaka 2009, baadhi ya wachezaji waliopita kwenye mikono yake wakati huo ni pamoja na Mezut Ozil, Toni Kroos, Khedira, Neuer na Hummels

Lakini pia Kaze amewahi kufanya kazi pale Hispania kwenye Academy ya Fc Barcelona, akiwa miongoni mwa wataalam katika shule hiyo
Katika Taifa lake la Burundi, Kaze alifundisha timu za Taifa kuanzia ngazi ya vijana mpaka timu ya wakubwa
Mwaka 2012 alitajwa kuwa kocha bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
Ni mmoja wa wataalam wanaotajwa kuweka msingi mzuri kwa soka la Burundi, mwaka jana timu hiyo ikifanikiwa kucheza fainali ya michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza katika historia yao

Ana leseni ya CAF daraja la kwanza (A) na pia ana leseni ya DFB inayotolewa na Shirikisho la soka kule Ujerumani

Post a Comment

0 Comments